Thursday , 29 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Moil yafunga biashara Tanzania, yahamia Uganda, DR Congo
Habari MchanganyikoTangulizi

Moil yafunga biashara Tanzania, yahamia Uganda, DR Congo

Mmiliki wa Kampuni ya mafuta ya Moil, Shanif Mansoor
Spread the love

KAMPUNI ya mafuta ya Moil, inadaiwa kuwa imeanza kuondoa biashara zake za uuzaji wa mafuta nchini na kuzihamishia katika nchi za Uganda na Congo kwa kile kinachotajwa kuwa kwa sasa Tanzania mazingira ya uwekezaji sio mazuri. Anaripoti¬†Mwandishi wetu … (endelea).

Moil inatajwa kumilikiwa na mbunge wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza, Shanif Mansoor (CCM) na Altaf Mansoor (Dogo), ambao wanamiliki vituo vya mafuta kadhaa hapa nchini.

Taarifa za ndani kutoka katika kampuni hiyo zinaeleza kuwa wamiliki wa kampuni hiyo wamelazimika kuondoa biashara nchini kutokana na mazingira ya kiuwekezaji kwa sasa nchini siyo rafiki.

Chanzo hicho cha ndani kutoka katika kampuni hiyo kinameueleza mtandao huu kuwa, kwa sasa tayari magari makubwa ya mafuta ya kampuni hiyo yamebadilishwa usajili wa namba za Tanzania na sasa zimesajiliwa kwa usajili wa nchi za Uganda na DR Congo.

“Wakurugenzi wao wanasema Tanzania sasa hivi biashara siyo nzuri na ufanyaji wake umekuwa mgumu na faida hakuna hivyo wamelazimika kuanza kuondoa biashara zao na kuzihamishia katika nchi za Uganda na DR Congo,” kilisema chanzo hicho.

Pia chanzo hicho kimebainisha kwamba uongozi wa kampuni hiyo ulikuwa umeanza kuondoa biashara zake nchini kwa muda mrefu lakini kwa gari hizo kumi za usafirishaji mafuta, usajili wa namba zake ulianza Februari 27 mwaka huu.

Kampuni ya Moil, ambayo ina vituo vya mafuta vitatu jijini Mwanza, inadaiwa kwa sasa gari inayosambaza mafuta kwenda jijini humo ni moja tofauti na awali zaidi ya gari kubwa za mafuta kuanzia 10 zilikuwa zikisambaza kwenye vituo hivyo.

Aidha chanzo hicho kimeendelea kudai kuwa pamoja na wanahisa wengine kushinikiza kuondolewa kwa biashara zao nchini pia mbunge wa sasa wa jimbo la Kwimba amekuwa akidai kuwa hana mpango wa kugombea tena ubunge mwaka 2020.

Kutoendelea kwa Mansoor katika nafasi hiyo pia kunadaiwa kuchangia kuhamishwa kwa Biashara za kampuni hiyo kwenda nchi hizo.

Mmoja wa wakurugenzi hao, Shanif Mansoor alipotafutwa kwa njia ya simu zaidi ya mara nne kwa nyakati tofauti ili kuzungumzia suala hilo, simu yake ya mkononi iliita bila majibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Hatutazuia watu kuingia barabarani

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kuruhusu vyama...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

error: Content is protected !!