December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MOI kugawa miguu bandia 600 bure

Hospitali ya Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI)

Spread the love

TAASISI ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), imetangaza kutoa bure miguu bandia 600 kwa watu wenye ulemavu wa miguu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 5 Aprili 2019 na taasisi hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter, inaeleza kwamba, zoezi la ugawaji miguu hiyo litaanza mwezi Mei mwaka huu.

Taarifa hiyo imewataka wenye uhitaji wa miguu hiyo wafike ndani ya mwezi Aprili kwa ajili ya vipimo.

“MOI kwa kushirikiana na Taasisi ya BMVSS ya India tutaendesha zoezi la kutoa miguu bandia 600 BURE. Wenye uhitaji wafike MOI ndani ya mwezi April 2019 kwa vipimo. Miguu hiyo itatolewa mwezi May 2019,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

error: Content is protected !!