August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mohammed Ali afariki dunia

Spread the love

MOHAMMED Ali, aliyekuwa bondia wa kwanza maarufu na mwenye asili ya Kiafrika, Raia wa Marekani, amefariki leo asubuhi.

Bondia huyo amefariki leo akiwa na umri wa miaka 74. Taarifa kutoka kwa msemaji wa familia yake, bondia huyo amefariki katika Jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.

Bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu, anajulikana sana kote duniani kutokana na historia yake katika mchezo wa ngumi.

Mohammed alikuwa na matatizo ya kupumua, hali ambayo ilitatanishwa zaidi na maradhi ya Parkinson (ugonjwa wa kutetemeka tetemeaka).

Taarifa ya familia yake imesema kuwa, ibada ya mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky.

Mohammed alipozaliwa, alipewa jina la Cassius Marcellus Clay.

Alipata umaarufu mkubwa aliposhinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyiwa Roma mwaka 1960 katika uzani wa uzito wa kadri (light-heavyweight).

Alipewa jina la Utani “The Greatest” na alimtandika makonde Mmarekani mwenzake Sonny Liston mwaka wa 1964 na kushinda taji lake la kwanza la Dunia.

Alikuwa bondia wa kwanza kushinda taji la uzito wa juu mara tatu. Alistaafu mwaka 1981 baada ya kushinda mashindano 56 kati ya 61 aliyoshiriki.

Kundi la waandishi wa habari wa michezo lijulikanalo kama Sports Illustrated lilimtaja kama “Mwanariadha wa Karne” ambapo BBC imemtambua kama “Mwanariadha mashuhuri zaidi wa Karne”.

Mohammed alijulikana sana kwa usemi wake wa kutangulia pigano au baada ya pigano. Aliweza kubashiri matokeo ya masumbwi kwa ustadi wa kuchapana makonde pia.

Pia bondia huyu alikuwa mkereketwa wa haki za kibinadamau ambapo atatambuliwa kukabiliana na ubaguzi wa rangi na ushairi wa kuvutia.

Alipoulizwa kama angetaka kukumbukwa vipi alisema wakati mmoja: “Kama mtu ambaye hakuwahaini watu wake. Na ikiwa hilo haliwezekani basi nijulikane tu kama mwanandondi mzuri.

Sijali hata usipotaja nilivyokuwa mwenye umbo la kuvutia.”

error: Content is protected !!