RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Uteuzi huo unetangazwa tarehe 1 Oktoba 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhurw Yunus.
“Uteuzi huu unaanza mara moja,” imeeleza taarifa ya Yunus.
Matinyi anachukua nafasi ya Gerson Msigwa, aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Msemaji huyo mpya wa Serikali, alishawahi kuwa mwandishi wa habari kwa miaka mingi katika vyombo mbalimbali vya habari, likiwemo Gazeti la kila siku la Majira.
Leave a comment