January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MOAT yakomalia muswada wa habari

Mwenyeki wa MOAT Dk. Reginald Mengi

Spread the love

WAKATI  Serikali ikiendelea kuweka vikwazo na kutaka kupitisha muswada wa vyombo vya habari kwa nguvu, Wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania (MOAT), wamesema wanauhakika kwamba  hautapitishwa Bungeni pasipokujadiliwa upya. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, imebainika, Serikali imeondoa kinyemela  Muswada wa vyombo vya habari katika Bunge linaloendelea hivi sasa na kupenyeza muswada mwingine wa sheria ya upatikanaji wa habari.

Akizungumza katika mkutano wa MOAT uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyeki wa MOAT Dk. Reginald Mengi amesema, muswada huo  haujakubalika kwani bado unakandamiza waandishi wa habari.

Mengi amesema  sheria ya upatikanaji wa habari bado itawanyima uhuru wa usambazaji wa habari kwa vyombo vinavyomilikiwa na watu binafsi ambalo ni kinyume cha katiba ya nchi.

“Kinachoshangaza ni kwanini serikali inazidi kutunga sheria ambazo kwa upande mmoja inabana? Wakati  ibara ya 5 kifungu cha (1) kinasema kila mtu anahaki ya kupata taarifa iliyochini ya wenye taarifa na kwamba kila mwenye taarifa atatoa taarifa ambayo ipo chini ya mamlaka yake” amesema Mengi.

“Sheria hizi bado zinamkanganyiko mkubwa hazieleweki upeo wa serikali hii kwa upeo wangu serikali inajaribu kuuzima uhuru wa kukusanya na kusambaza habari kwa wananchi” amesema Mengi.

Amesema  endapo muswada huo utapita nchi hii itakuwa katika hatari ya kupata habari zisizorasmi, kutokana kwamba watoa habari hawatakuwa huru.

 Nae Rostam Aziz mmoja kati ya wajumbe wa MOAT ameisisitiza Serikali kutopeleka muswada huo bungeni  unaweza kuleta sheria mbaya nchini na kandamizi.

“Sisi kama MOAT tunatamka sauti moja kwamba tutahakikisha muswada huu hautapitapitishwa hadi serikali itakapoamua kurudi nyuma na kutushirikisha wadau wote ndipo utapitishwa.”. amesema Rostam.

error: Content is protected !!