February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

MO Dewji awaombea mema Yanga

Spread the love

MWEKEZAJI wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ amewataka wanachama na viongozi wa klabu ya Yanga kuungana upya, ili kuinusulu klabu katika kipindi hiki cha mpito ambacho kinawakabili kutokana na ukata wa fedha pamoja na wimbi la viongozi kujiuzuru. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mo ametoa ujumbe huo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, uliosomeka: “Tunahitaji Yanga imara ambayo inaweza kushindana na Simba. Tunahitaji Yanga imara kwa ajili ya timu bora ya Taifa Stars. Ninawaombea Yanga waweze kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, wanapaswa watulie na waungane upya.”

Kauli hiyo imekuja baada ya wachezaji wa klabu hiyo juzi kugomea mazoezi kwa kushinikiza kulipwa malimbikizo ya mishahara yao ya nyuma,  pamoja na kujiuzuru Katibu wake, Charles Mkwasa na Msemaji, Dismass Ten, huku wanachama wakitaka makamu mwenyekiti wao Clement Sanga kujiudhuru kwa kushindwa kuiongoza klabu.

Yanga imeonekana kuwa katika hali hii mbaya ya kiuchumi toka alipojiweka pembeni aliyekuwa Mwenyekiti klabu hiyo, Yusuf Manji, licha ya wanachama kumtaka arudi katika nafasi yake hiyo ya mwenyekiti katika mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Juni 10, 2018.

error: Content is protected !!