December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

MO Dewji apewa Urais wa Heshima Simba

Mohammed Dewji ‘Mo’

Spread the love

 

BODI ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, imemteuwa Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ kuwa Rais wa klabu hiyo mara baada ya kujiudhuru nafasi yake ya mwenyekiti wa Bodi wa klabu hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa hii leo tarehe 21, Novemba 2021 kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere na Mwenyekiti wa sasa wa bodi hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again.’

Katika hotuba yake kiongozi huyo alisema, kutokana na kikao cha bodi kilichofanyika hivi karibuni na mchango mkubwa aliotoa kwa klabu hiyo, wameamua kumpa Urais wa Heshima, Mo Dewji.

“Kwa kutambua mchango mkubwa kwenye klabu yetu na kutokana na kikao cha bodi tuilichokaa hivi karibuni, tumeamua kumpa urais wa heshima Mohammed Dewji ‘MO.’ alisema Salim Abdallah.

Kiongozi huyo aliendelea kuwahakikishia wanachama wa klabu ya Simba waliojitokeza kwenye ukumbi huo kuwa, mwekezaji huyo bado yupo ndani ya klabu ya Simba na hivyo kila kitu kipo sawa.

 

Mo alijiuzuru nafasi yake ya uwenyekiti wa bodi kwa kile alichokieleza kuwa, amekuwa akibanwa na shughuli nyingi hivyo muda mwingi anakuwa safarini nje ya nchi na nafasi hiyo akaikabidhi wa Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye ndiyo mwenyekiti kwa sasa.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo alisema kuwa, kwa sasa timu yao ipo imara licha ya kuwa na presha nyingi kutoka kwa mashabiki lakini wachezaji wamepambana na kuhakikisha wanapata matokeo na kuwataka mashabiki watulie.

“Tuna timu imara, pamoja na presha nyingi kutoka kwa washabiki vijana wetu waliweza kupambana kuhakikisha wanapata matokeo kwenye wakati mgumu, Presha ilikuwa kubwa, Tulieni,” alisema Try Again.

Try Again amesema hayo kufuatia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting  uliochezwa kwenye dimba la Ccm Kirumba, Mwanza.

error: Content is protected !!