October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mo Dewji ang’oka Simba, ateua mrithi

Mohammed Dewji ‘Mo’

Spread the love

 

MOHAMED Dewji, Mkurugenzi wa Bodi ya Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ametangaza kuachia nafasi hiyo na kumteua Salim Abdallah ‘Try Again’ kuchukua nafasi yake. Anaripoti Damas Ndembela, TUDARCo … (endelea).

MO ametangaza uamuzi huo leo Jumatano, tarehe 29 Septemba 2021, akisema amekuwa na majukumu mengi yanayomfanya kuwa nje ya Tanzania jambo linalosababisha kutokutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Salim Abdallah ‘Try Again’

Bilionea huyo kijana Afrika amesema, Try Again aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bodi ana uwezo wa kutosha kusimamia jukumu hilo nna “mimi bado nipo, bado nitaendelea kujishirikisha kwa soka la vijana na kuboresha miundombinu na bodi itashughulika na timu.”

error: Content is protected !!