Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo MO Dewji akata Ngebe, aweka Bil 20
MichezoTangulizi

MO Dewji akata Ngebe, aweka Bil 20

Spread the love

Mfanyabiashara na mwekezaji ndani ya klabu ya Simba, Mohammed Dewji (MO), ameweka rasmi kiasi cha pesa shilingi 20 bilioni, kama sehemu ya uwekezaji ndani ya klabu ya Simba mara baada ya mchakato wa mabadiliko kukamilika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchakato huo wa mabadiliko ndani ya klabu ya Simba, ulidumu katika kipindi cha miaka minne, mpaka hivi karibuni ambapo tume ya ushindani (FCC), ilipotoa hati ya mchakato huo kukamilika na mwekezaji huyo, ambaye ni tajiri namba moja kijana barani Afrika kuweka pesa hiyo.

Mo Dewji ameweka kiasi hiko cha fedha kama manunuzi ya hisa zake asilimia 49, mara baada ya klabu hiyo kufanya mchakatao wa mabadiliko ya katiba Mei 2018 Kwa kuruhusu timu hiyo kwenda kwenye mfumo wa mabadiliko.

Akiwa mbele ya waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam, aliingiza pesa hiyo kwa kuonesgha mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 20 bilioni na kusema kuwa jambo hilo limeshaisha.

“Kwa leo hii tuna hafla ya kuweka hiyo Pesa, na leo natoa hiyo Shilingi 20 bilioni rasmi na nitatoa cheki hapa ili jambo hili liishe.” Alisema mwekezaji huyo

Aidha mfanya biashara huyo aliongezea kuwa katika kipindi cha miaka minne ambapo klabu hiyo ilikuwa inasubiri mchakato huo ukamilike, bajeti ya Simba ilikuwa ndogo na ilimlazimu yeye kutoa fedha ya ziada Zaidi ya shilingi 5.3 bilioni kwa mwaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yatoa tamko bungeni sakatala la viboko shuleni

Spread the love  SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na wilaya kuratibu...

error: Content is protected !!