Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko MO Dewji aelewa somo la JPM
Habari Mchanganyiko

MO Dewji aelewa somo la JPM

Spread the love

MOHAMMED Dewji ‘Mo’, Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (METL), amempongeza Rais John Magufuli kwa jitihada zake za kuleta mageuzi  katika sekta ya usafirishaji, viwanda na miundombinu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mo ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and Packaging Ltd  kinachomilikiwa na Kampuni ya METL.

Mfanyabaishara huyo ameeleza, wale wasiomuelewa Rais Magufuli watamuelewa baadaye kwa kushuhudia matokeo ya mageuzi anayofanya kupitia serikali yake.

“Tunakupongeza wewe binafsi na serikali yako kwa kufanya mageuzi makubwa, tuna uhakika wale wasiokuelewa sasa watakuelewa baadae. Na wasio elewa lengo lako, wataeleweshwa na matokeo yatakayokuja,” amesema Mo.

Amesema, miradi inayotekelezwa na Serikali ya Rais Magufuli ikiwemo mradi wa kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (Stigler’s Gorge), ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge) pamoja na barabara, itarahisisha gharama za uzalishaji na usafiurishaji wa bidhaa za viwanda.

 “Sisi jumuiya ya wawekezaji tumefurahishwa na uwekezaji kwenye reli, barabara na majuzi tumekuona ukizindua mradi wa Stigler. Kwetu wenye viwanda ni faida kubwa kwani uwekezaji wetu unaathiriwa na bei kubwa ya umeme na ukatikaji umeme.

Lakini mradi huu utawezesha kupata umeme wa uhakika. umeme huu utakua na unafuu kwa wenye viwanda na walaji wetu kwa hili nakupongeza sana,” amesema Mo.

Pia amezungumzia ununuzi wa ndege saba za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), akisema kwamba hatua hiyo itaimarisha sekta ya usafiri wa anga, pamoja na kuvutia watalii.

“Haijawahi kutokea kwenye nchi yetu kwamba tumenunua ndege saba katika kipindi cha miaka miwili. Watanzania tumekuwa wanyonge kwenye utalii ukilinganisha na wenzetu Kenya.

“Licha ya kuwa na vivutio vingi Kenya wana shirika la ndege imara. mimi kijana wako na utajiri wangu wote nimeshindwa hata kununua ndege yangu binafsi,” amesema Mo .

Rais Magufuli amemtoa wasi wasi Mo kwamba serikali yake iko tayari kuwaunga mkono wawekezaji kwa lengo kuimarisha sekta binafsi.

“Mo Dewji endelea wala usiwe mnyonge chapa kazi Tanzania iko pamoja na wawekezaji wanaojenga viwanda. Nasema kwa dhati kazi unayofanya ni nzuri,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema, viwanda vipya takribani 4,000 vimejengwa nchi nzima, tangu alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2015

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!