November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MO Dewji adaiwa kutekwa alfajiri ya leo

Spread the love

MFANYABIASHARA Mohammed Dewji, anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto leo saa 11 Alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi Gym ya Colosseum, Oysterbay Dar es salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, inasemekana watu hao wamefyatua risasi hewani kuwatishia watu walikuwa karibu na eneo hilo kabla ya kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ameeleza kuwa Jeshi hilo linafuatilia utekwaji wa Mfanyabiashara huyo.

error: Content is protected !!