May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mo Dewji aahidi makubwa Simba

Mohamed Dewji (MO), Mwekezaji wa klabu ya Simba

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba ya Dar es salaam, nchini Tanzania, Mohamed Dewji ‘MO’ amepanga kuwekeza fedha zaidi ndani ya timu hiyo ili iweze kufanya vyema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mo Dewji, ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, tarehe 16 Mei 2021, kupitia akaunti yake ya Twitter, ikiwa ni siku moja kupita, tangu kushuhudia, Simba ikishushiwa mvua ya magoli 4-0 dhidi ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini.

Kipigo hicho, ilikipata kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika na cha kwanza kikubwa kwenye michuano hiyo kwa msimu wa 2020/21.

Ili kusonga mbele, Simba itahitaji kushinda goli 4-0 ili kuingia dakika 30 za nyongeza au kushinda 5-0, katika mchezo wa marudiano, utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Mo Dewji amesema, starehe yake haitakuwa na maana kama Simba haitakuwa ikifanya vizuri na mpango wake wa kujizawadia magari ya kifahari aina ya Ferrari na Rolls-Royce ameusitishwa kwanza.

“Nilipanga kujizawadia Ferrari na Rolls-Royce, sina budi kuweka mpango huu kapuni kwa sasa na kuelekeza fedha zaidi katika klabu yetu ya @SimbaSCTanzania. Furaha ya @SimbaSCTanzania ni muhimu kuliko starehe yangu. Simba kwanza!,” amesema Mo Dewji.

error: Content is protected !!