Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Michezo ‘MO’ awarahisishia kazi wachezaji Simba
Michezo

‘MO’ awarahisishia kazi wachezaji Simba

Mohamed Dewji 'MO Dewji'
Spread the love

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba na mwekezaji mkuu wa timu hiyo Mohammed Dewji ‘MO’ ametangaza kiingilio cha shilingi 2000, kwenye mchezo wa klabu bingwa katika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly kutoka nchini Misri, utakao chezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Mchezo huo wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi unatarajiwa kupigwa 12 februari, 2019 majira ya saa 10 kamili jioni ambapo amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi licha ya kupata matokeo mabaya kwenye mchezo ulipita.

“Tumepanga kiingilio cha shilingi 2000 kwa majukwaa ya mzunguko ambapo mechi ya mwanzo kiingilio kilikuwa ni shilingi 5000. Kesho asubuhi tutatangaza rasmi viingilio vyote vya mechi yetu na Al Ahly siku ya Jumanne”.

“Kwenye mpira huwezi kuchukua lift upande juu lazima upande ngazi, nawaomba Wanasimba tusivunjike moyo wote tumeumia, huo ndo mpira, Mi naona tuna nafasi, tulishawahi kuwafunga Al Ahly hapa nyumbani” alisema ‘MO’

Lengo la simba kuweka kiingilio hicho kinaweza kufanya watu wengi kujaa uwanjani na kuishangilia timu hiyo kwani matokeo pekee ya ushindi kwenye mchezo huo ndio yanayoweza kuwapa simba matumaini ya kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali.

Hata hivyo mwekezaji huyo amekili ya kuwa kwa sasa Simba inashindana na timu ambazo zinauwekezaji mkubwa barani afrika na kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye suala kama usajiri kwa wachezaji.

“Ukiongelea Al Ahly unaweza kuilinganisha na Real Madrid kwenye mataji, juzi wamenunua mchezaji kwa zaidi ya Bilioni 10 na huyo mchezaji ametoa assist zaidi ya tatu kwenye mechi tuliocheza nao” aliongezea ‘MO’

Ikumbukwe Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza katika mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly kwa mabao 5-0 kwenye mchezo uliochezwa jijini Alexadria, Misri.

Simba ambayo ipo kwenye D inashika nafasi ya tatu na alama tatu baaada ya kushinda katika mchezo wa awali dhidi ya JS Saoura kutoka Algeria na baadae kukumbana na kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa AS Vital ya Congo.

Al Ahly ambao wametwaa kombe hili mara nane, kuingia fainali mara tisa na vinara wa kundi hilo wanatarajia kuanza safari siku ya kesho februari 9 kuja nchi kuivaa Simba siku ya jumanne na kama watafanikiwa kushinda mchezo huo basi watakuwa wamefuzu moja kwa moja kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Michezo

Unamalizaje Jumapili hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Jipigie pesa na Meridianbet leo hii

Spread the love KAMPUNI kubwa ya ubashiri Tanzania inakwambia hivi huu ndio...

Michezo

Endelea kubashiri na Meridianbet, Ligi bado zipo

Spread the love BAADA ya ligi mbalimbali kutamatika, bado kuna ligi mbalimbali...

error: Content is protected !!