Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko MO ahofia yatima wa Kibonde, Kikwete: Jahazi litaendeleaje?
Habari Mchanganyiko

MO ahofia yatima wa Kibonde, Kikwete: Jahazi litaendeleaje?

Spread the love

WAKATI maandalizi ya kuupumzisha mwili wa aliyekuwa mtagazaji wa Redio ya Clouds,Ephraim Kibonde baada ya kufariki dunia jana asubuhi tarehe 7 Machi 2019 yakiendelea, mfanyabiashara bilionea nchini Mohamed Dewj (MO) ameonesha hofu yake kwa watoto wa mwanahabari huyo. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Kwenye ukurasa wake wa Instagram mfanyabiashara huyo ameandika majonzi yake baada ya kufariki kwa Kibonde aliyetanguliwa na mama wa watoto hao (mkewe) aliyefariki miezi minne iliyopita.

MO ameandika: “Nawawaza watoto wake, wamebaki yatima, Mungu awape nguvu. Pumzika kwa amani Kibonde, Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.”

Viongozi wengine wa nchi na wastaafu wameendelea kuonesha masikitiko yao baada ya taarifa za kufariki Kibonde kuthibitishwa na familia, taasisi aliyokuwa akiitumikia (Cloudes Media) pamoja na hospitali.

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ameguswa kwa namna yake ambapo

kwenye ukurasa wake wa Twitter “Majonzi yangali nasi, nimepokea taarifa ya kifo cha mtangazaji Ephrahim Kibonde wa Clouds. Ni pigo kubwa kwetu sisi wapenzi wa kipindi cha Jahazi,” ameandika Rais Kikwete na kuongeza;

“Jahazi litaeleaje bila ya Nahodha Kibonde? Mwenyezi Mungu na aipe faraja familia yake, Clouds na wasikilizaji wote wa Jahazi.”

Miongoni mwa waliotoa pole ni Ally Hapi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye aliandika kwenye Intagram: “Hakika inatosha kifo kuwa ni mawaidha tosha kwa wanadamu. Kama mpenzi wa kipindi cha Jahazi la Clouds, tutammiss sana brother Kibonde kwa ucheshi, umahiri na kipaji chake cha pekee.

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika ukurasa wake wa Instagram ameandika “Poleni sana Clouds kwa pigo hili kubwa! Hakika mnapitia katika kipindi cha majaribu.

Judith Wambura ‘Lady J Dee’, Msanii wa bongo Fleva nchini ameandika katika Instagram “Hili ni jambo zito kwa watu wenye ukaribu na Ephraim Kibonde. Tunakaa tunakunywa, tunacheka siku nyingine mmoja wetu anatwaliwa.”

Baada ya Kibonde kufariki, video (clip) moja imekuwa ikisambaa kwa kasi ambapo anaonekana kueleza maneno yaliyofanana na kile kilichomtokea.

“Sisi binadamu hatuna lolote kwenye ulimwengu huu. kama si leo kesho, kama si kesho basi keshokutwa. Huwezi kujua muda gani na siku gani wakati wake utafika, safari yake itakuwa imefika,” ni maneno aliyoeleza kutokana na msiba wa Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG).

Kibonde alifariki dunia jana asubuhi jijini Mwanza wakati akipelekwa katika Hospitali ya Rufani ya Bugando kutoka hospitali ya Uhuru jijini humo.

Kibonde anatajwa kusumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu wakati. Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema,  familia ya Clouds imepata pigo lingine kubwa kwa kuondokewa na mfanyakazi wao Kibonde baada ya Ruge.

Mwili wa Kibonde umewasili Dar es Salaam jana usiku na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo tayari kwa ajili ya kuagwa kesho Jumamosi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!