October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mnyika: Tunataka tume huru, nguvu ya umma haijawahi kushindwa

Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, ameitaka Serikali kutumia kipindi kifupi kilichobaki cha uhai wa Bunge, kupeleka muswada wa maberebisho ya sheria yatakayowezesha uwepo wa tume huru ya uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Bunge la 11 lililozinduliwa tarehe 20 Novemba 2015 na Rais wa Tanzania, John Magufuli, anatarajia kulihutubia kwa mara ya mwisho tarehe 19 Juni 2020 jijini Dodoma.

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema, akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano tarehe 3 Juni, 2020 makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, amesema kwa ratiba mpya ya Bunge, kuna mwanya mdogo umebaki kabla kuanzia tarehe 5 hadi 10 Juni 2020 ikiwa ni siku moja kubaki kabla ya kusomwa kwa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2020/21.

Mnyika amesema “Kuna ka mwanya kadogo kamebaki” hivyo Rais wa Tanzania John Magufuli na Bunge wapeleke muswada bungeni utakaoifanya kuwepo na tume huru ya uchaguzi.

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema

“Uchaguzi huru, haki na wa amani kwa njia ya kistaarabu. Tunafuatilia yote yanayoendelea. Tumejifungia ndani na tunawaambia watawala, tunataka tume huru ya uchaguzi,” amesema Mnyika.

“Mikakati tutakayoitumia na njia tutakazozitumia wasitulaumu kwa sababu ‘People Power’ (nguvu ya umma) haijawahi kushindwa,” amesema.

Amesema, katika muda muafaka, tutawaongoza wananchi kudai haki yao kupitia sanduku la kura.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo Jumatano na Ofisi ya Bunge, inaonyesha kutakuwa na miswada itakayowasilishwa kuanzia tarehe 5 hadi 10 Juni 2020.

error: Content is protected !!