Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika: NEC turudishieni wagombea ili tupimane ubavu
Habari za SiasaTangulizi

Mnyika: NEC turudishieni wagombea ili tupimane ubavu

Spread the love

JOHN Mnyika, Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwarejesha wagombea wao wa madiwani na wabunge ili wapimane ubavu na vyama vingine. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mnyika alitoa kauli hiyo jana Ijumaa tarehe 4 Septemba 2020 katika mkutano uzinduzi wa kampeni Kanda ya Kati inayohusisha mikoa ya Singida, Dodoma na Morogoro uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Uhuru jijini Dodoma uliofanywa na Lissu.

Akihutubia umati wa wananchi kwenye mkutano huo, Mnyika aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhakikisha inatenda haki na kutupilia mbali mapingamizi waliyowekewa wagombea ubunge na udiwani ili waweze kupimana mabavu katika sanduku la kura.

Alisema, katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 ameamua kutogombea ubunge wa Kibamba jijini Dar es Salaam ili kujenga chama kutokana na kuona jinsi Bunge la 11 lilivyoendeshwa na Spika Job Ndugai.

“Mimi kwa sasa siyo miongoni mwa wabunge walioweka historia ya kustaafu siasa si kwamba nisingeweza kushinda ubunge Kibamba lakini nimeamua kustaafu ili kujenga chama hasa baada ya kuona jinsi Bunge linavyoendeshwa na Spika Job Ndugai.”

“Nimeweza kukaa na marais kama vile Jakaya Kikwete na Rais (John) Magufuli na kuwatafakari. Pia, nimekaa na Lissu naye nimemtafakari hakika hakuna rais bora kama Lissu, kati ya marais waliotangulia hivyo wanadodoma na Watanzania msifanye kosi kutomchagua Tundu Lissu ili awe rais wa nchi hii,” alisema Mnyika.

Naye mgombea mwenza wa urais, Salum Mwalimu alisema ni fahari kubwa kwake na wanadodoma kumpata makamu wa Rais kutokea Dodoma tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

“Mimi ni mtoto wa Dodoma, shule ya msingi nimesoma hapo shule ya Msingi Mlimwa na sekondari nimesoma shule ya sekondari ta Dodoma.”

Mgombea mwenza wa urais Chadema, Salum Mwalimu

“Kwa maana nyingine, mimi ni mtoto wenu, naomba mnichague niwe makamu wa Rais ili niweze kuwa makamu wa Rais naomba kura nyingi mpeni Tundu Lissu ili awe rais pamoja na wabunge na madiwani,” alisema Mwalimu.

“Kura za kimbunge zimwendee Tundu Lissu ili aweze kuwa rais wa Tanzani, wanadodoma, tumekuwa tukipakwa mafuta na mgongo wa chupa, wanadodoma maisha ni magumu kutokana na kutufanya sisi ni jiji lakini wao wanazidi kupiga dili,” alisema Mwalimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!