Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika awatumia ujumbe wasaidizi Rais Samia
Habari za Siasa

Mnyika awatumia ujumbe wasaidizi Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

CHAMA kikuu cha siasa nchini Tanzania cha Chadema, kimeendelea kusisitiza umuhimu wa majadiliano baina yao na Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan ili kupata mwafaka bora wa kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 28 Oktoba 2021 na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi mbalimbali wa chama hicho Kanda ya Pwani inayoundwa na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yenyewe.

Lengo la mkutano huo ni kumbukizi ya mwaka mmoja kupita tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoka 2020.

Mnyika amesema, pamoja na madhira yote waliyopita na wanayopitia ikiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kufikisha siku 100 akiwa gerezani, lakini kuna umuhimu wa kufanyika kwa majadiliano.

“Pamoja na mapito yote tuliyopitia kama chama baada ya uchaguzi, bado hatukufunga milango ya majadiliano na mwenyekiti Freeman Mbowe alimwandikia barua Rais Samia. Ni miezi sita sasa imepita tangu Rais aingie madarakani na hajasema lini yatafanyika,” amesema Mnyika.

Mnyika amewaomba wasaidizi wa Rais na walio karibu naye kumkumbusha umuhimu wa majadiliano kwani yataliteta taifa pamoja kuliko hivi ilivyo sasa.

Amesema, wataendelea kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya hata kama Mbowe ataendelea kushikiliwa au Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara akiwa nje ya nchi.

“Kuendelea kumshikilia Mbowe, haiturudishi nyuma. Mbowe awe gerezani, (Tundu) Lissu awe nje ya nchi bado tutaendelea kudai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi bila kukoma,” amesema

“Tume huru ya uchaguzi ni nyezo ya kupata viongozi makini. Sheria zikipitishwa na Rais akiisaini chanzo ni uchaguzi. Tukiangalia matatizo mengi ni ya kiuongozi na mfumo. Hata tutayaepuka kama tukiwa na tume huru, itakayowezesha kupata viongozi bora,” amesema.

Mnyika amesema ni mwaka mmoja umepita tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu “leo ni mwaka mmoja umepita tangu tulipofanya uchaguzi 28 Oktoba 2020. Tukumbuke kwa machungu tulikotoka na tukumbuke tunakokwenda ili Taifa letu lisirudishwe tulipotoka kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi.”

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu aliwashukuru Watanzania wote kwa ushirikiano wote waliowaonesha wakati wa kampeni hizo.

Mwalimu amesema, “nawashukuru sana wanawake namna mlivyoshiriki uchaguzi mkuu 2020. Tulikuwa na wagombea 58 wanawake kuliko chama chochote kwenye uchaguzi huo. Hakika uchaguzi ulikuwa mzuri sana.”

1 Comment

  • Asante ndugu mnyika taifa.la tanzania ni moja na watanzania wapo pamoja na wanao uwezo wa kudumisha umoja na hasa pale wanapoona kuna mtu anauchukia umoja wa tanzania ndugu mnyika fikiria yenye kuleta maendeleo yako na ya chama chako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

Habari za Siasa

Ushindi wa mpinzani Senegal wakoleza moto kwa wapinzani Tanzania

Spread the loveUSHINDI wa aliyekuwa mgombea  urais wa upinzani nchini Senegal, Bassirou...

error: Content is protected !!