Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika amkabili Spika Ndugai
Habari za Siasa

Mnyika amkabili Spika Ndugai

Spread the love

JOHN Mnyika, Mbunge wa Kibamba jijini Dar es Salaam amepinga hatua ya Job Ndugua, Spika wa Bunge kufukuza wabunge kwa madai ya kudhalilisha Bunge. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Amemueleza Spika Ndugai kwamba, heshima ya Bunge haijengwi kwa kuwafukuza wabunge, kuwadhalilisha wabunge na kuwaadhibu wabunge kama ambavyo utaratibu huo umekuwa ukizoeleka.

“Heshima yoyote ya Bunge haiwezi kulindwa kwa kufukuza wabunge wake, kuwaadhibu wabunge wake, kuwadhalilisha wabunge wake na kuwahukumu wabunge wake.

“Heshima ya Bunge italindwa kwa Bunge kutumia vizuri madaraka yake. Na kwetu yamewekwa kwenye Katiba ibara 63 (2) kuhusu mamlaka ya kusimamia, kuishauri serikali, kuisimamia serikali na kuwawakilisha wananchi, ndio Bunge lenye heshima kwa wananchi,” amesema Mnyika baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasilisha ripoti leo tarehe 4 Aprili 2019.

Ripoti hiyo imewasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka na baadaye Bunge kuazimia Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kwa kuunga mkono kwamba, Bunge ni dhaifu.

Akichangia baada ya ripoti hiyo Mnyika amesema, katika mazingira kama haya, mapendekezo na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Bunge ya Maadili zikataliwe na kuwa, zinaendelea kudhalilisha Bunge.

Mnyika amesema, kanuni ya 8 (a) inamtaka spika kuendesha Bunge bila chuki wala upendeleo. “Sasa nini kilitokea, ndio maana nasema mapendekezo yote ya kamati yanapswa kutupiliwa na Bunge.”

“Nitanukuu kauli ya Lema, Lema akasema, mimi ni mbunge wa vipindi viwili, nathibitisha Bunge hili ni dhaifu. Mara baada ya Lema kumaliza maneno hayo, Naibu Spika kinyume na kanuni ya 5 (1) , 5 (2) ya Bunge akasimama akasema, Lema kwa maneno hayo uliyosema na wewe unapelekwa kamati ya maadili,” amesema Mnyika.

Kabla ya Mnyika kuhitimisha, Spika Ndugai aliingilia kati kwa kusema, “naombeni leo wala kusiwe na taarifa, tuwaache waseme, watumie dakika zao 10 na wao, wangine watasema dakika zao 10, leo sitaki fujo. Anayeleta fujo leo, hamna cha taarifa wala nini, endelea…’

Mnyika amesema, kama utaratibu huo wa kutaka kulinda hadhi ya Bunge ungefuatwa, Lema angetakiwa kufuta kauli au athibitishe pale pale bungeni.

“Na kama angeshindwa kuthibitisha, utaratibu ambao ungefuata ni uko kwenye kanuni ya 63 (9) ambapo kanuni pekee zilizotajwa kama ni kosa la kwanza, kukosa vikao 10. Utaratibu ungekuwa tofauti na mapendekezo ya kamati,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!