Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika amgomea Waziri wa JPM
Habari za SiasaTangulizi

Mnyika amgomea Waziri wa JPM

Spread the love

JOHN Mnyika, Mbunge wa Kibamba (Chadema) amepinga kauli ya Juma Aweso, Naibu Waziri wa Maji kwamba, jimbo hilo limesambaziwa maji kwa asilima 80. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Katika majibu yake aliyotoa leo tarehe 8 Aprili 2019 katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma, Aweso amesema, asilimia 80 ya wananchi wa Kimbamba wanapata huduma ya maji.

Jibu hilo limepingwa na Mnyika akidai kuwa, ni uongo kwa kuwa asilimia kubwa ya kata zilizoko katika jimbo hilo hazina maji.

Mnyika amedai kuwa, kata nyingi zilizoko kwenye jimbo lake hazina miuondombinu ya maji ikiwemo mabomba ambapo amemtaka Aweso kutoa takwimu halisi ya upatikanaji wa maji jimboni mwake.

“Katika majibu yake naibu waziri amesema, asilimia 80 ya wananchi wa Kibamba wanapata maji ya bomba, jambo ambalo ni taarifa ya uongo inayotolewa bungeni.

“Sababu kuna maeneo mengi hayana mabomba ya maji, kwa kuwa waziri ametoa jibu la uongo, yuko tayari kutoa takwimu halisi ya upatikanaji wa maji Kibamba mtaa kwa mtaa?” amesema Mnyika.

Akijibu swali la Mnyika, Aweso amemhoji Mnyika kwamba, yeye kama Mbunge wa Kibamba hajui mitaa yenye maji, yeye kama waziri atajuaje?

Amemtaka Mnyika afanye ziara katika jimbo lake ili aone kazi ya usambazaji maji inayofanywa na serikali.

“Nimhakikishie kwamba, serikali imefanya kazi kubwa sana, kipindi cha nyuma kulikuwa na mgawo lakini kwa sasa kuna ugawaji wa maji kwa asilimia 85. Sasa kama mbunge hujui mitaa yako yenye maji, mimi nitajuaje?

“Nakushauri uende kwenye jimbo lako, niko tayari kuambatana na wewe nikakuonyeshe kazi nzuri iliyofanya na CCM. Mheshimiwa spika anayejua mihemeo ya mgonjwa ni anayelala na mgonjwa,” amesema Aweso.

Piam Mnyika alihoji kwamba, Wizara ya Maji imechukua hatua gani kutokana na kauli ya hivi karibuni ya Rais John  Magufuli katika ziara yake ya mikoa ya kusini kuhusu changamoto ya miradi hewa ya maji?

“Rais akiwa ziarani alisema, wizara ya maji ina mainjinia wanapafom ovyo ovyo na miradi hewa. Kwa kuwa rais ameshatoa hii kauli, na ni agizo, je wizara iko tayari taarifa iliyotolewa na rais ili tuchukue hatua ya miradi hewa nchini?” amehoji Mnyika.

Akijibu swali hilo, Aweso amesema, wizara ya maji imeanza kufanyia kazi changamoto hiyo ikiwemo kwa kuwafuta kazi wahandisi wasiotekeleza wajibu wao.

“Kuhusu kusua sua kwa miradi, wizara tumekuwa tukichukua hatua kwa wababaishaji tumejipanga kuchukua hatua, wahandisi wababaishaji hawana nafasi nawachukulia hatua na tumeanzisha wakala wa maji vijijini ili kuchukua kushuhulikia changamoto za maji.,” amesema Aweso.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!