Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika acharukia hati ya dharura
Habari za SiasaTangulizi

Mnyika acharukia hati ya dharura

John Mnyika, Mbunge wa KIbamba (kushoto). Kulia ni Job Ndugai Spika wa Bunge
Spread the love

MBUNGE wa Kibamba John Mnyika (Chadema) amepinga kitendo cha rais Dk.John John Magufuli kupeleka hati ya Dharura ya kupitisha mswada wa sheria ya madini na mafuta na gesi, anaandika Dany Tibason.

Mnyika amecharuka muda mfupi baada ya spika wa Bunge Job Ndugai kueleza kuwa amepokea mswada wa  sheria ya Madini, mafuta na gesi kutoka kwa rais ili uweze kufika bungeni kwa hati ya dharura.

Mnyika akiomba mwongozo wa Spika muda mfupi baada ya spika kutoa maelezo yake amesema ni kwanini miswada hiyo mitatu isijadiliwe katika bunge lijalo.

“Muda mfupi uliopita tumekabidhiwa ratiba ya bunge, serikali inaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura, mwaka 1997 mikataba ya madini ilipitishwa harakarahaka, mikataba ya ngesi hivyo hivyo, kazi ya bunge ni kutunga sheria, sisi ndio wawakilishi wa wananchi, kama sisi wawakilishi wa wananchi kwanini  hii miswada mitatu kwa umuhimu wake na maslahi yake kwa ananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa kukutana na wananchi, ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza na hati ya dhrarura ikaondolewa ikaletwa bunge lijalo”alihoji Mnyika.

“Kwa maelezo uliyotoa kwanini wadau wasiitwa kwa short notisi wafike Dodoma kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichaambue, mheshimiwa spika huu ni mtego kwa kutufanya tushindwa kuishauri serikali kwa kutimiza kazi yetu ya kibunge.

“Mapendekezo haya yatenguliwe , miswada hiyo ijadiliwe katika bunge lijalo” alisema Mnyika.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama amesema Masharti ya kutunga sheria na masharti ya jumla yamewekwa katika fasihi ya nane ya kanuzi za bunge, masharti yameongezwa na kanuzi ya 80 na kanuni nyingine, miswada ambayo imeletwa imekuja katika hati ya dharura, ili bunge liridhie kama miswada hiyo inastahili kujadiliwa na bunge ama la.

“Kanuni 80(4) inasema mswada wowote wadharura haiutaingizwa katika shughuli za bunge bila kuwa na hati iliyowekwa sahihi na rais kuthibitisha kwamba muswada huo ni wa dharura.

“Kanuni zinaendelea kusema kuwa iwapo kamati inaona muswada wa sheria wa serikali uliowasilishwa kwa hati ya dharura haustahili kamati hiyo ya uongozi itaishauri serikali.

“Kanuni zinaendelea kusmea, muswada wowote uliokabidhiwa kwako spika utaonekana unastahili ama la, utatoa picha na baadaya kujadiliwa na kamati.

“Sisi kama serikali tumeshatimiza masharti yote ndani ya bunge lako tukufu, tumeshakamilisha hatua zote za kufikishwa muswada huo kwa hati ya dharura.

“Wanaoweza kulishauri bunge baada ya kuona uzito wa kazi iliyoletwa na serikali ni kamati husika itakayopewa kazi ya kujadili miswada hiyo.

“Haitakuwa busara sisi wabunge kabla hatujaona yaliyomo katika miswada hiyo tukajenga hoja ndani ya bunge ya kukataa maslahi mapana ya taifa letu bila kuangalia kilichomo ndani ya miswada, hata wabunge tulioko upande mwingine wa bunge pia tunawawakilisha wananchi” amesema Mhagama.

Awali Spika wa Bunge Jobu Ndugai alisema kwa niaba ya wabunge amepokea hati ya dharura kutoka kwa rais Dk.John Magufuli.

“Kanuni zinasema itakuja hati yenyewe yenye sahihi yake, hati ya dharura imekuja kuna haja ya kulifanyia jambo hili kazi, tulijadiliana na kamati ya uongozi tukakubaliana na suala hili ili lisonge mbele.

“Tumeunda makundi mawili, kamati moja ya kawaida na kamati ya pili ina kamati nne ndani nyake, watakaa katika ukumbi wa Pius Msekwa kuanzia leo mchana, kuanzia leo.

“Wakati rais akipokea ripotinya pili makinikia (mashapo), kwa niaba yenu nilikubali kama kuna mambo yenye maslahi kwa nchi tukayafanyia kazi, mambo yameletwa katika kamati husika, kamati itajadili kama miswada inastahili kuingia bungeni ama la hoja nitatokea huko.

“Bunge linatakia kuwa na nafasi fulani katika masuala yanayohusu maadini na gesi, liwe na nafasi fulani ili kuzuia nchi kuingia kutumbikia katika mikataba mibovu” alisema Ndugai.

Aidha amesema miswada iliyowasilishwa bungeni ataipaata katika tovuti.

Miswada mitatu mipya iliyowasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza ni muswada wa sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti hasi katika mikataba ya maliasili za nchi wa mwaka 2017, muswada wa sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa maliasili wa maka 2017 na muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali zenye upungufu uliojitokeza wa mwaka 2017.

“kamati ya uongozi ilikaa jana(juzi) kubadilisha ratiba kamba Bunge litaahirishwa Julai 5 badala ya Juni 30 kama ilivyokuwa , miswada mitatu mipya ya sheria imesomwa kwa mara ya kwwanza, itapelekwa katika kamati za Bunge.

Muswada wa kwanza wa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali zenye upungufu uliojitokeza wa mwaka 2017 utafanyiwa kazi na Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohammed Mchengelwa wakati mikataba mingine miwili itafanyiwa kazi na kamati ya pamoja itakayoongozwa na Dotto Biteko ambapo ndani yake kuna kamati nne.

Ngugai alizitaja kamati hizo  nne kuwa ni Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Kamati ya Sheria ndogo ndogo na Kamati ya Katiba na Sheria.

Amesema kamati hizo zitafanya kazi kuanzia jana kisha taarifa itawasilishwa bungeni, Kamati itapanga jinsi ya kukutana na wadau mbalimbali na Bunge litaahirishwa Julai 5 mwaka huu.

“Kamati itapanga jinsi ya kukutana na wadau mbalimbali” alisema Spika.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!