July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mnigeria wa Stand atua Coastal Union

Abasarim Chidiebele akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United, Abasarim Chidiebele amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya Coastal Union kwa mkataba wa miaka mmoja katika msimu ujao wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Chidiebele atua mkoani Tanga juzi kwa ajili ya kuingia makubaliana na uongozi wa timu ya Coastal Union ambapo utiliaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi, Meneja wa Coastal Union, Akida Machai na viongozi wengine.

Akizungumza mara baada ya kusaini, Chidiebele amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na Coastal Union na kuhaidi kutumia uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao.

“Nashukuru kusajili Coastal Union kikubwa niwahaidi tu wapenzi,wanachama na mashabiki kutumia uwezo wangu katika kuipa mafanikio timu yetu “Alisema Mshambuliaji huyo ambaye ni tishio hapa nchini.

Kwa upande wake,Ofisa Habari wa Klabu ya Coastal Union, Oscar Assenga alisema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakaowawezesha kuhakikisha wanachukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

“Unajua usajili wetu sio wa kukurupuka hivyo lazima tuwe makini kwani hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kuhakikisha tunatimiza mipango yetu ya kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao “Alisema.

Hata hivyo aliwataka wapenzi mashabiki kuweka mshikamano wa pamoja ambao utatuwezesha kufanikisha malengo yao ya mwakani kushiriki kombe la shirikisho kwa kuanza kufanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu.

error: Content is protected !!