October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Mnasema Rais ni mweupe! dokoa pesa muone rangi halisi’ – Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia amewaonya viongozi, watumishi na wazabuni watakaosimamia miradi itakayotekelezwa kwa kutumia fedha zilizotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa Tanzania, basi wajaribu kudokoa fedha hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Oktoba, 2021 jijini Dodoma wakati akizindua mpango wa kampeni ya maendeleo kwa ustawi na mapambano ya UVIKO -19 ambao umetokana na mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika hilo la IMF.

“Hili niliseme tu kwa wale wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi mkinitazama hivi mnasema Rais ni mweupe lakini nina rangi halisi, kwa wale wanaotaka kujua rangi zangu halisi, wajaribu kudokoa pesa hizi au wabadilishe matumizi ya pesa hizi bila maelewa,” amesema.

Aidha, amesema kutokana na mpango huo nchi inakwenda kuchemka, kila kona kutakuwa na ujenzi, miradi ya maendeleo hivyo wakurugenzi wa halmashauri na wasaidizi wao wasimamie miradi hiyo ipasavyo kuhakikisha fedha hii inatumika ipasavyo.

error: Content is protected !!