July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mmoja afariki dunia, nane waokolewa baada ya kufunikwa machimboni

Spread the love

MTU mmoja amefariki duniani wakati nane wakinusurika kifo baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya madini wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo tarehe 10 Septemba 2019, ambapo watu 10 walikumbwa na mkasa huo na mmoja kupoteza maisha.

Kamanda Jumanne Murilo, kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza amethibitisha tukio hilo akisema kwamba juhudi za kumuokoa mtu mmoja aliyebaki zinaendelea.

“Tukio hilo limetokea kweli, mtu mmoja amepoteza maisha, nane wameokolewa, juhudi zinaendelea za kumuokoa mmoja aliyebaki katika machimbo hayo,” amesema Kamanda Murilo.

error: Content is protected !!