August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mmisri aliyeitia hasara TCRA kizimbani

Spread the love

NAGER OSMAN (64) raia wa nchi ya Misri amepandishwa kortini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mashitaka ya kuitia hasara ya zaidi ya Sh. 200 milioni serikali ya Tanzania, anaandika Faki Sosi.

Raia huyo amedaiwa kuisababishia hasara serikali ya Tanzania kutokana na kuendesha mitandao bila kibali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa nchini (TCRA).

Akisoma mashitaka hayo Adolfu Mkini Wakili wa Serikali mbele ya Wilbard Mashauri Hakimu Mkazi katika Mahakama hiyo amedai kuwa mtuhumiwa huyo alijishughulisha na shughuli za kuendesha mitandao bila kibali cha TCRA kati ya 19 Mei mpaka 20 Julai mwaka huu.

“Mtuhumiwa huyo alitenda makosa kati tarehe 19 Mei  2016 na 20 Julai 2016  ambapo  aliendesha mitandao ya mawasiliono ya kieletroniki na kutumia mkonga wa Taifa bila ya leseni ya TCRA,” amedai Mkini.

Mkini ameeleza zaidi kuwa mtu huyo ameisababishia serikali hasara ya zaidi Sh. 203,949,000 ambapo akiwa Upanga jijini Dar es Salaam, akitumia  mfumo wa GSM VOIP isivyo halali.

Katika hali iliyozua vicheko, mtuhumiwa huyo alishindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea mahakamani hapo kutokana na kutoelewa lugha ya Kingereza wala Kiswahili.

Hata hivyo, mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo kwa hiyo mtuhumiwa hakutakiwa kujibu mashitaka hayo.

Hakimu Mashauri amemtaka Mwendesha Mashtaka kutafuta mkalimani wa lugha anayotumia mtuhumiwa huyo ambayo ni Kiarabu.

Kesi hiyo itatajwa tena terehe 25 Agosti Mwaka huu.

error: Content is protected !!