October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mmiliki wa Shamba Mahagi adakwa na polisi kwa kuchochea vurugu mgodini

Spread the love

 

JESHI la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mmiliki wa shamba, Gelvas Bambo pamoja na wenzake watatu kwa kosa la kufanya vurugu na kuchoma gari la mwekezaji wa Mgodi wa Mahagi uliopo katika kijiji cha Izunya Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita. Anaripoti Paul Kayanda, Nyang’hwale … (endelea).

Eneo linalogombaniwa ni lile machimbo ya madini ya dhahabu ambapo lina ukubwa wa urefu wa mita 50 kwa mita 30 huku eneo jingine la ukubwa wa ekari 3 likiwa wazi bila mgogoro wowote baina ya wamiliki hao wawili.

Akizungumza jana tarehe 20 Disemba, 2021 kwa njia ya simu Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo lilitokea hivi karibuni kwenye Mgodi wa Mahagi uliopo katika kijiji hicho.

Kamanda Mwaibambe alisema hatua hiyo inatokana na mgogoro uliopo katika eneo la uchimbaji wa madini ya dhahabu baina ya wamikiki wa mashamba pande mbili baada ya mfumuko wa madini hayo.

“Mgogoro huo upo mahakamani, uamuzi wa mahakama ni kwamba shughuli za uchimbaji zisitishwe kwanza kwenye eneo hilo lakini pia kwa pande hizo mbili mmoja ameshinda anapaswa apate mgao wake,” alisema.

Alisema vurugu zilitokea wakati wa ugawaji wa mawe yanayosadikiwa kuwa na madini ya dhahabu ndipo mzee Bambo hakukubali mawe yabebwe mpaka wote wamalize kesi.

“Ni kweli watu wanne tunawashikilia akiwemo mzee Bambo kwa kufanya vurugu zilizosababisha gari la mwekezaji kutaka kuchomwa moto pamoja na familia yake kwa lengo la kishinikiza mifuko ya mawe yanayosadikiwa kuwa na madini aina ya dhahabu yasitolewe kwenye eneo lake mpaka mahakama ikapotoa idhini ya nani mshindi,” alisema.

Naye mmiliki mwingine wa shamba, Iddrisa Hussein pamoja na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika eneo hilo walitumia fursa hiyo kumuomba Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Kimadini Mbogwe mhandisi Joseph Kumburu aruhusu kuendelea kwa shughuli za uchimbaji wa Madini hayo kwa kuwa wachimbaji hawapo sehemu ya mgogoro.

Pia Iddrisa alisema licha ya kwamba shamba lake lilikuwa na mgogoro mzito hakuweza kukwamisha shughuli za uchimbaji kama alivyokwamisha Bambo hivyo anamuomba RMO huyo kuufungua mgodi huo uendelee kufanya kazi kwani madini ni mali ya serikali mtu mmoja asikwamishe.

Aidha, Kaimu mwenyekiti wa Mgodi wa Mahagi, Joseph Yabita alikiri kuibuka kwa mgogoro huo ambao almanusura gari la mwekezaji anayesimamia leseni kuchomwa moto.

Akijibu hoja hizo afisa Madini Mkazi wa mkoa wa kimadini Mbogwe, Mhandisi Joseph Kumburu alisema eneo linalogombaniwa na wamiliki hao wa mashamba baada ya mashamba yao kuibuka na dhahabu ni lile lenye uchimbaji wa madini.

Alisema eneo hilo lina urefu wa mita 50 kwa mita 30 huku eneo jingine la ukubwa wa ekari 3 likiwa wazi bila mgogoro wowote baina ya wamiliki hao wawili.

Afisa Madini huyo alisema kuwa sababu kubwa iliyopelekea afunge mgodi huo ni kutoelewana wamiliki wa mashamba na fujo wanazozifanya wakati wa ugawaji wa mawe yanayosadikiwa kuwa na madini ya dhahabu.

“Vurugu zilitokea wakati maafisa wa madini wakitekeleza majukumu yao ya kugawa mawe yanayosadikiwa kuwa na madini ya dhahabu baada ya mmoja kati ya wamiliki wa mashamba kupewa ruhusa ya kuchukua mali yake baada ya kushinda kesi.

“Siyo kwamba tumeruhusu uchimbaji kwani kesi nyingine bado ipo mahakamani,” alisema Joseph Kumburu.

error: Content is protected !!