
Lee Jae-yong aliyetarajia kurithi kampuni ya Samsung, akiwa chini ya ulinzi baada ya kuhukumiwa
MRITHI aliyetarajia kurithi kampuni ya Samsung, Lee Jae-yong amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na mahakama ya nchini Korea Kusini kwa kosa la rushwa, anaandika Jovina Patrick.
Lee ambaye pia anafahamika kama Jay Y Lee na kiongozi wa kampuni hiyo kubwa zaidi ya kutengeneza simu duniani, amekuwa kizuizini tangu mwezi februari akikabiliwa na tuhuma kadhaa za rushwa.
Miongoni mwa makosa aliyokabiliwa nayo ni utoaji rushwa, wizi wa mali ya umma na kuficha mali nje ya nchi.
Wakili wa Lee amesema watakata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo,”Tuna imani kwamba hukumu hii itabatilishwa,” wakili Song Wu-cheol amewaambia wanahabari baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo.
Hata hivyo, uamuzi huo wa mahakama ni pigo kubwa kwa kampuni hiyo kubwa zaidi na inayofahamika zaidi duniani.
More Stories
Uholanzi, Uturuki ‘waingia’ vitani
Mauaji ya Jamal Khashoggi, CIA yaivua nguo Saudia Arabia
Marekani yafanya ‘uchochezi,’ yawaonya wanaokuja Tanzania