May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mmbape hati hati dhidi Man City leo

Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa PSG, Kylian Mmbape huenda akaokosa mchezo wao dhidi ya Manchester City leo, baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Parc De Princes jijini Paris. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utapigwa hii leo kwenye dimba la Etihad jijini Manchester mara baada ya PSG kupoteza kwa mabao 2-1, kwenye mchezo wa awali.

Mmbape ambaye alipata majeruhi ya kifundo cha mguu, alikosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa dhidi ya Lens ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa kikosi cha PSG, Mauricio Pochettino alinukuliwa akisema kuwa watamuangalia afya ya mchezaji huyo kwenye mazoezi kabla ya mchezo huo.

Mmbape mpaka sasa ameshapachika jumla ya mabao nane, kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu akiwa kwenye nafasi ya pili, nyuma ya mshambuliaji wa Borrusia Dortmund, Erling Haaland ambaye ana mabao 10.

PSG chini ya Pochettino wanaingia kwenye mchezo huo wa leo huku wakiwa nyuma kwa mabao 2-1, wanahitaji ushindi wa mabao 3 kwa bila ili waweze kufuzu kwa hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Kwa upande wa Manchester City ambayo ipo chini, Pepe Guardiolla wamekuwa na rekodi nzuri wakiwa nyumbani kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika michezo mitano waliocheza Manchester City kwenye Uwanja wa Etihad kwenye michuano hiyo wamefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo yote.

error: Content is protected !!