August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mlipuko watokea uwanja wa ndege Brussels

Spread the love

WATU 11 wanahofiwa kufariki dunia, wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili kwenye Uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels, nchini Ubelgiji.

Bado haijafahamika chanzo cha milipuko hiyo, lakini moshi mkubwa umetanda katika maeneo ya kukaguliwa abiria waoandoka.

Watu wameanza kuondolewa katika uwanja huo, kwa kunusuru usalama wao.

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba watu 11 wanahofiwa kufariki na wengine kujeruhiwa katika ukumbi wa kuhudumia watu wa safari za kuondoka nchini na kwamba milipuko ilitokea karibu na meza ya shirika la ndege la American Airlines.

error: Content is protected !!