September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mlipuko wa Corona: Wapinzani waishauri Serikali

John Mrema, Mkurugenzi wa Itikadi Uenezi na Mawasiliano Chadema

Spread the love

VYAMA vya siasa vya upinzani nchini vimeitaka Serikali kuchukua hatua za makusudi, katika kuhakikisha mlipuko wa Ugonjwa ya Homa ya Mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19), unadhibitiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Chama Kikuu cha Upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia kwa John Mrema, Mkuu wake wa Itifaki na Mambo ya Nje, kimeitaka serikali kusambaza vifaa vya kupima ugonjwa huo katika hospitali zote za mikoa, wilaya na za mipakani.

Pia, izuie raia wa kigeni kuingia nchini, hasa wanaotoka katika mataifa yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huo, vifaa vya kujikinga vitolewe na mamlaka husika badala ya kuuzwa na watu wasiokuwa na utaalamu juu ya amsuala ya afya, ili kuepusha mamabukizi mapya.

Hali kadhalika Chadema imeshauri serikali kudhibiti misongamano ya watu katika maeneo ya vituo vya mabasi,  polisi, hospitali, mahakamani pamoja na kuweka vifaa vya kupimia na sabuni za kunawia mikono.

“ Watanzania hawana Akiba ya chakula. 5.Serikali itume ndege Addis Ababa kuchukua vipimo 20K na Mask 100K vilivyotolewa na Jack MA kwa nchi za Africa kwa ajili ya madaktari na wahudumu wa afya ambao wako hatarini zaidi kuathirika. 6.Kuzuia mikusanyiko, Masokoni, ibada na shuleni,” amesema Mrema.

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameishauri serikali kununua chakula cha kutosha ili nchi iwe na akiba ya kutosha katika ghala la taifa la chakula. Ili kudhibiti ongezeko la bei za vyakula.

“Naishauri Serikali kukutana na Wafanyabiashara wote kwenye sekta ya Utalii na Vyama vya Wafanyakazi kwenye sekta hiyo, kwa lengo la kupata tathmini ya pamoja ya madhara ya mlipuko huu kwa sekta ya Utalii na huduma zake.

Serikali itazame namna ya kuwafidia ( stimulus package) wafanyabiashara katika sekta hiyo, ili kulinda ajira za Wananchi. Ikiwezekana fidia iwe ni kulinda ajira kwa kufidia gharama za wafanyakazi ( payroll costs),” ameshauri Zitto.

Wakati huo huo, Zitto amemshauri Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, kuwasilisha bungeni taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Corona kwa uchumi wa Tanzania, ili ijadiliwe kwa ajili ya kutoa mapendekezo ya kibajeti.

“Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona kwa Uchumi wa Tanzania kwa ujumla, na Bunge lijadili Kwa maslahi ya Taifa ili kutoa mapendekezo ya kibajeti kuhami Uchumi wa Nchi yetu na haswa kulinda biashara ndogo, Wafanyakazi kwenye sekta zilizo hatarini kama Utalii, huduma za vyakula, usafirishaji na uchuuzi.

error: Content is protected !!