Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mlipuko mabomu Afghanistan waua 60, majeruhi 140
Kimataifa

Mlipuko mabomu Afghanistan waua 60, majeruhi 140

Spread the love

 

WATU takribani 60 wameuawa huku 140 wakijeruhiwa, katika milipuko ya mabomu iliyotokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai Mjini nchini Afghanistan. Inaripoti BBC Swahili…(endelea).

Milipuko hiyo imetokea jana Alhamisi tarehe 27 Agosti 2021, katika uwanja huo uliokuwa unatumia na baadhi ya wananchi waliojaribu kutoroka nchi hiyo wakiwakimbia wanamgamboi wa Taliban.

Kwa mujibu wa mtandao huo, miongoni mwa watu 60 waliofariki dunia katika milipuko hiyo ni maafisa 12 wa kikosi maalum cha Jeshi la Marekani. Pia, maafisa wengine 15 wa jeshi hilo walijeruhiwa.

Awali, mataifa ya magharibi yalionya wananchi waukwepe uwanja huo baada ya taarifa za kiintelijensia kubaini kuna shambulio la mabomu liliandaliwa na Kitengo cha Afghanistan cha kundi la Islamic State.

Kwa mujibu wa BBC Swahili, mlipuko wa kwanza ulitokea majira ya jioni karibu na Hoteli ya Baron, iliyopo karibu na uwanja huo, ambayo ilikuwa inatumiwa na maafisa wa Uingereza, waliokuwa wanaratibu mipango ya raia wa Afghanistan wanaotaka kwenda nchini kwao.

Mlipuko wa pili ulitokea karibu na lango la uwanja wa ndege huo, linalofahamika kwa jina la Abbey Gate.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!