August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mlinzi ajeruhi kwa risasi

Spread the love

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Bernad Amon (30), Mlinzi wa Kampuni ya Quick kwa tuhuma za kufyatua risasi kwa uzembe na kusababisha majeraha kwa watu wawili, anaandika Christina Haule.

Katika tukio hilo waliojeruhiwa ni Ramadhan James (21) Mkazi wa Nanenane ambaye alijeruhiwa kichwa, kifuani na mguu wa kushoto na Hussein Ally (27), Mkazi wa Kilakala ambaye alijeruhiwa mguu wa kushoto.

Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amesema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi  saa 11:45 jioni kwenye Barabara ya Boma wakati mlinzi huyo akifanya ukaguzi wa bunduki yake aina ya Shotgurn.
Amesema kuwa, wakati mlinzi huyo akiendelea na ukaguzi gafla  alifyatua risasi kabla ya kumkabidhi mlinzi mwenzake lindo, hata hivyo majeruhi wanaendelea vizuri.
Amesema kuwa, mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake  ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

error: Content is protected !!