August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mlinda mlango wa Chapecoense astaafu soka

Jose Nivaldo, kipa wa Chapecoense

Spread the love

MLINDA mlango wa klabu ya Chapecoense, Jose Nivaldo (42) ametangaza kustafu mchezo wa soka kufuatia ajali ya ndege iliyotokea nchini Colombia juzi nakupoteza maisha ya baadhi ya nyota na viongozi wa klabu hiyo walipokuwa wakienda kucheza mchezo wa kwanza wa fainali dhidi ya Atletico National.

Golikipa huyo ambaye hakusafiri na timu katika mchezo wa raundi ya kwanza wa fainali za Copa Sudamericana uliokuwa ufanyike nchini Colombia, kutokana na kujiandaa kucheza mchezo wake wa 300 akiwa na klabu yake hiyo mwishoni mwa wiki dhidi ya Atletico Mineiro ili aweze kutundika daruga.

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo klabu mbalimbali ulimwenguni na baadi ya wachezaji wameendelea kutoa rambirambi zao kwenda kwa timu hiyo ambayo mpaka sasa imesalia na wachezaji sita tu, watatu kati ya hao ndio walionusurika kwenye ajali na wengine hawakusafiri kabisa.

Baadhi ya timu nchini Brazil zinampango wa kutoa baadhi ya wachezaji kwenye vikosi vyao vya kwanza kwa ili kwenda kuongeza nguvu kwenye klabu hiyo na huku wakiwa na maombi maalumu kwa shirikisho la soka nchini humu ya kutoishusha timu hiyo daraja kwa kipindi cha miaka mitatu kwa ajili ya kupewa muda wa kujipanga zaidi.

Lakini pia klabu ya Palmeiras ambayo imeshatangazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi nchini humo nao wamepeleka maombi maalumu kwenye shirikisho lao kwa ajili ya kutumia jezi za Chapecoense kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kwa ajili ya kuwakumbuka wenzao waliopoteza maisha kwenye ajali ya ndege.

error: Content is protected !!