March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mlimani City watoa sababu za kufungia Nakumatt

Milango ya duka la Nakumatt likiwa imefungwa

Spread the love

DUKA kubwa (Supermarket) la Nakumatt lililopo jijini Dar es salaam, limelifungia, baada ya kukosa bidhaa za kutosha kwa muda mrefu pamoja na kudaiwa kodi za huduma mbalimbali, anaandika Angel Willium.

Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastory Mroso ameuambia MwanaHALISI Online, kuwa wamechukua uamuzi huo baada ya duka hilo kushindwa kutimiza vigezo walivyowekea ikiwa pamoja na kupewa notisi miezi minne kufanyia marekebisho tatizo hilo.

Mroso amesema pamoja na kuwapa notisi hiyo lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, wakawaongezea tena notisi ya mwisho ya siku kumi ambayo ilikuwa inaisha siku ya Jumamosi, na kuamua kuwafungia asubuhi ya leo.

Meneja huyo ameendelea kwa kusema kwamba tatizo hilo limekuwa likiwaathiri wafanyakazi na hata bidhaa za wafanyabiashara wengine na wamelishalitolea taarifa serikalini kwa hatua zingine zaidi.

error: Content is protected !!