
Mkwe wa Osama bin Laden, Sulaiman Abu Ghaith
Sulaiman Abu Ghaith amehukumiwa kifungo cha maisha siku ya jumanne wiki iliyopita. Haya yalisemwa na msemaji wa ofisi ya mwanasheria wa serikali huko manhattan. Ghaith alizaliwa mwaka 1965 na ameoa mtoto wa Osama bin Laden.
Mwezi wa tatu mwaka huu Ghaith alionekana na makosa ya ugaidi kwa kusaidia al Qaeda, ikiwa ni pamoja na njama za kuua wamarekani na kutoa msaada wa vifaa kwa magaidi. Abu Ghaith, 48, alisafirishwa mwaka mmoja uliopita kutoka Jordan na akafunguliwa kesi ya kufanya njama ya kuwaua wamarekani
“Haki imepatikana” Mwanasheria mkuu wa Marekani alisema “matokeo ya kesi hii yatasababisha Ghaith, kiongozi wa ngazi ya juu wa al Qaeda na mshirika wa Osama bin Laden, kutopata nafasi tena kukanyaga ardhi nje ya magereza.”
Marekani imemtaja Ghaith kuwa alikuwa mtengeneza “waziri wa propaganda” na ni sauti na sura ya al Qaeda siku chache baada ya September 11.
Wakati wa kusomewa hukumu yake, msomaji mashitaka alisema Ghaith msomi wa dini wa Kuwait, alikuwa na jukumu kubwa la kupanga mipango na mikakati, msemaji mkuu na mkufunzi wa wanamgambo, akisaidia “utunzaji wa hazina ya magaidi wapya” baada mipango ya mauaji kugeuza wafuasi wake kuwa wafiadini.
Gaith alikuwa zaidi ya Usoma, baada ya shambulio la 9/11 alichukua nafasi kama muuaji kwa kuwashawishi wafuasi wa al Qaeda kuwaua wamarekani.
Mshauri wa Kiroho wa bin Laden
Gaith alitoa ushahidi kuwa hajawahi kujiunga na vyeo vya al Qaed bali alimsadia Bin Laden kama mzungumzaji wa mambo ya kiroho.
Gaith akiwa ghuba ya Uajemi (Persian gulf), alikuwa mkufunzi wa dini na mzungumzaji mwenye ushawishi. Juni 2011 alikutana na kiongozi wa al Qaeda huko Afghanistan. Wakati anatoa ushahidi wake alikataa kuwa alifahamu kinachoendelea kabla ya shambulio la September, hata hivyo alisema alisikia ikiongelewa kuwa “kitu kikubwa” kitatokea.
Gaith alihama na familia yake kutoka Afghanistan kwenda Kuwait kabla ya shambulizi la Sep 11, 2001, shambulizi lililotokea katika majengo ya New York’s Trade Center na Pentagon.
Mara baada ya shambulio hilo kiongozi wa al Qaeda alimuita Abu Ghaith kwenye sehemu yake ya maficho huko milimani-Afghanistan na akatakwa kutoa ujumbe kwa Dunia kwa niaba ya al Qaeda. Ghaith alisema wakati akitoa ushahidi.
Mwaka jana Gaith alikamatwa huko Jordan, baada ya kukamatwa wanaharakati na wanasheria walikomaa juu ya wapi afunguliwe mashitaka. Baadhi walitaka kesi yake isikilizwe Guantanamo Bay-Cuba. Badala yake kesi ilifanyika kwenye mahakama ya wilaya huko Manhattan.
Mahakama hiyo imeangalia mikanda ya video, iliyorekodiwa baada ya Ghaith kukutana na kiongozi wa al Qaeda. Katika mkanda huo Gaith alionekana kuwa na hisia kali na kushawishi mashambulizi zaidi kwa waamerika, huku pembeni yake akiwa na bin Laden na upande mwingine akiwa na AK-47.
Mkanda huo ulionyesha Gaith akiwataka waislamu kuwapa hofu makafiri na kuapa kwamba “mvua ya mabomu haita simama” maelezo aliyojitetea kuwa alipewa na bin Laden kuyatamka akiwa ameshikiliwa bunduki.
Mtetezi mwanasheria wa Ghaith alimlaumu mtaja mashtaka kwa kutumia kivuli cha September 11 badala ya ushahidi wa mteja wake.
More Stories
Kesi mauaji ya Jamal Khashoggi yaanza tena
Angola, Rwanda, DRC, Rwanda, Kenya zanufaika chanzo ya corona
Uholanzi, Uturuki ‘waingia’ vitani