Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Mkwasa, Bocco wang’aa tuzo za mwezi Ligi Kuu
Michezo

Mkwasa, Bocco wang’aa tuzo za mwezi Ligi Kuu

Boniface Mkwasa, Kocha wa Ruvu Shooting
Spread the love

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Simba, John Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa Novemba, huku kocha wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa akichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi huo, kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Tuzo hizo utolewa kila mwezi wakati wa msimu wa Ligi Kuu ambazo zipo chini ya kamati maalumu ya Ligi Kuu chini ya usimamizi wa bodi ya Ligi.

Bocco ameshinda tuzo hiyo mara baada ya kuwashinda kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Deus Kaseke pamoja na mshambuliaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Abdulrahaman Mussa.

Ndani ya Novemba Simba ilicheza michezo mitatu na kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mechi mbili huku Bocco akifunga mabao matatu (hat-trick) kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ambao Simba waliibuka na ushindi wa mabao 7-0.

Kwa upande wa Mkwasa alishinda tuzo hiyo, baada ya kuwashinda Mecky Mexime anayekinoa kikosi cha Kagera Sugar sambamba na Fulgence Novatus wa Gwambina FC ambao wote waliingia fainali.

Wachezaji ambao mpaka sasa wameshashinda tuzo hiyo toka kuanza kwa Ligi msimu huu 2020/21 ni mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube ambaye alishinda tuzo hiyo Oktoba na kiungo mkabaji wa Yanga, Tonombe Mukoko.

Huku kwa upande wa makocha walioshinda tuzo hiyo, ni aliyekuwa kocha wa Azam FC, Alistica Cioaba ambaye alishinda tuzo hiyo Septemba na kocha wa Yanga Cedric Kaze aliyeshinda tuzo hiyo Oktoba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!