July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkwasa apewa mkataba wa kudumu Stars

Spread the love

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars,’ Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa kudumu kukinoa kikosi hicho  kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika  Machi 31, 2017.

TFF Imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa baada ya kurudhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.

Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.

Naye kocha Mkwassa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda.

Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.

error: Content is protected !!