Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil
Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu (kulia) akizindua vyumba vya madarasa
Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba sita vya madarasa katika shule ya Msingi Kinyangwa iliyopo Kijiji Cha Katunduru kata ya Ilima wilayani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Mradi wa ujenzi wa vyumba hivyo umetekelezwa na Kampuni ya Bioland kupitia Mradi wa Cocoa for School kwa garama ya Sh. 64 milioni huku wananchi wakichangia nguvu zao kwa zaidi ya milioni 30.

Kampuni ya Bioland hujishughulisha na ununuzi wa zao la Kakao na faida yake huirejesha kwa jamii Kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Akizundua madarasa hayo leo, Haniu ameishukuru kampuni hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuwa kufanya hivyo itaongeza ufaulu katika shule hiyo baada ya mazingira ya kusomea na kujifunza kuboreshwa.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia hivyo wadau mbalimbali pamoja na wananchi hawana budi kumuunga mkono sambamba kutunza miundombinu ya elimu ili ikinufaishe kizazi hiki na kijacho.

Haniu ameagiza wazazi wote katika kijiji hicho kujitokeza na kuchangia chakula cha mchana shuleni ikiwa ni nyenzo imara ya kuongeza ufaulu sanjari na kuondoa udumavu na utapiamlo kwa watoto.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Renatus Mchau ameeleza kuwa ufaulu kwa wanafunzi wa elimu ya msingi umeendelea kupanda mwaka hadi mwaka kwa asilimia 93.7% (2022) na hii imechangia na ufundishaji mzuri wa walimu, ubora wa miundombinu ya kufundishia na chakula shuleni.

Hata hivyo  Mchau ameonya baadhi ya walimu kutumia muda wao vibaya badala ya kufundisha wanafunzi na hivyo kusababisha wanafunzi kukosa maarifa na ujuzi hatimaye kushindwa mitihani yao ya mwisho.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu

Katika hatua nyingine uongozi wa Kampuni ya Cocoa for School umeeleza kuwa utaendelea kuisaidia shule hiyo kwa kukarabati ofisi ya walimu pamoja na vyumba vingine vitatu vya madarasa vilivyobaki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!