Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkuu wa Wilaya ya Rungwe awakabidhi maafisa ugani pikipiki 61
Habari Mchanganyiko

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe awakabidhi maafisa ugani pikipiki 61

Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amekabidhi jumla ya pikipiki 61 kwa Maafisa Ugani katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha na kuongeza tija katika sekta ya kilimo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Akikabidhi pikipiki hizo, leo Machi 7, 2023, Haniu amewagiza wataalamu hao wa kilimo kwenda na kushiriki ipasavyo katika usimamizi na uzalishaji wa mazao ya kilimo ikiwa ni mbinu bora kuongeza kipato cha kaya na lishe kwa jamii.

Aidha, ameagiza pikipiki hizo kutumika kwa malengo mahususi yaliyokusudiwa ikiwa ni nyenzo sahihi ya kuwafikia wakulima kuanzia ngazi ya shina, Kitongoji hadi kijiji.

“Tahadhari msiende kutumia pikipiki hizi kama bodaboda mtakuwa mnakiuka malengo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wakulima wanapata ushauri wa kitaalamu na kwa wakati,” ameongeza Haniu.

Akishukuru kwa niaba ya maafisa ugani, Jenister Munisi mtaalamu wa kilimo kutoka Kata ya Kinyala amemshukuru Rais kwa maamuzi thabiti aliyoyafanya na kuwa wataenda kutekeleza kwa vitendo zoezi la uzalishaji wa mazao ya chakula biashara kwa ngazi ya kaya na jamii kwa jumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!