MKUU wa wilaya ya Kisarawe, Fatuma Almas Nyangasa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kituo cha michezo wilaya ya Kisarawe kesho smptemba 2, 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani …. (endelea).
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Pwani (Corefa), Mohamed Masenga alisema kituo hicho kitakuwa cha tatu kati ya vinne vya awali ambavyo itafikia saba kwa kila wilaya kimoja baadae kuongeza tena viwili kila wilaya na kutimia 21 mkoa mzima.
“Tunaweka vituo kwa ajili ya kuwafundisha vijana na watoto mpira wa kisasa na sheria za mpira wa miguu ili kuhakikisha wanakuwa wachezaji wazuri hapo baadae kwa faida ya mkoa na Tanzania nzima,” alisema Masenga.
Aidha Masenga alisema vituo hivyo vitakuwa chini ya FA za wilaya na mkoa kwa kushirikiana pamoja kwani corefa inatoa vifaa na walimu ili kuhakikisha fa wa wilaya wanawasukuma watoto na vijana chini ya miaka 8 hadi 20 waende kujifunza mpira wa miguu na sheria zake.
Hata hivyo vituo viwili vya awali tayari vishazinduliwa wilaya ya Kibaha na Mkuranga huku sasa zamu ya Kisarawe alafu baadae Rufiji na wilya zengine.
Mwisho amewataka wadau na wapenzi wa mpira wa miguu kuwaleta watoto wao majira ya saa mbili asubuhi ili kuhakiksha wanapata elimu ya soka na sheria kwani zoezi ni bure na endelevu kwa maslahi mapana ya soka la mkoa wa Pwani.
Leave a comment