February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mkuu wa Wilaya aagiza waliotapeli mamilioni wawekwe ndani

Pingu

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gift Msuya ameagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watu watatu wanaodaiwa kutapeli wananchi sita kiasi cha Sh. 6.5 milioni. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Watuhumiwa hao waliotambuliwa kwa majina ya Kulwa, Mayuga na Mang’ombe wanadaiwa kufanya utapeli huo tarehe 2 Novemba 2018.

Akizungumza baada ya kukutana na wakazi wa Igombe leo tarehe 5 Novemba 2018, Msuya amesema watu hao waliowarubuni wananchi hao, kwa kuwataka watoe fedha ili wakawasaidie kuwatolea dhamana baadhi ya watu waliokamatwa kwenye hifadhi ya Igombe.

“Kamanda OCS natoa maelekezo watu wote waliohusika kuwatapeli wananchi hawa hiyo milioni sita na nusu wakamatwe mara moja na wafikishwe kituo cha polisi,” ameagiza Msuya.

“Haiwezekani watu wengine wanaumia kutafuta hela kwa jasho, wengine wanakuja kula kwa mteremko. Mimi kama mtetezi wa wanyonge kama alivyo Rais wangu John Magufuli sitakubali jambo hili katika wilaya ninayoiongoza,” amesema.

error: Content is protected !!