June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkuu wa usalama Haiti mbaroni kwa mauaji ya rais

Jovenel Moise

Spread the love

 

MKUU wa Usalama nchini Haiti, Jean Laguel Civil, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Jovenel Moise. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Moise aliuawa kwa kushambuliwa na risasi tarehe 7 Julai 2021, akiwa mapumzikoni katika makazi yake binafsi, yaliyoko kwenye Milima ya Port-au-Prince, nchini humo.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi la Haiti, Civil anahojiwa kufuatia tukio hilo, akidaiwa kwamba alikula njama na watu waliomuuwa Moise.

Inadaiwa kuwa, Civil aliruhusu wauawaji hao kuingia katika makazi ya Moise, usiku wa manane, bila ya walinzi wa rais huyo kujua.

Kwa sasa mkuu huyo wa usalama amewekwa kizuizini gerezani, katika Mji wa Delmas, ulioko karibu na Mji Mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Haiti, Marie Michelle Verrier, amesema Civil alikamatwa Jumatatu, tarehe 26 Julai 2021, akiwa sehemu ya uchunguzi wa mauaji hayo.

Kamishna wa Port-au-Prince, Bed-Ford Claude, ameagiza mamlaka ya uhamiaji kudhibiti mipaka ya mji huo, ili kuzuia Polisi wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo, wasitoroke .

Hadi sasa Polisi nchini Haiti wanawashikilia raia 20 wa Colombia, wanaodaiwa kutekeleza mauaji hayo baada ya kukodiwa na mahasimu wa Moise.

error: Content is protected !!