
Mji wa Bamenda nchini Cameroon
MKUU wa shule pamoja na wanafunzi wa kiume 79 wametekwa nyara na makundi ya waasi katika jiji la Bamenda nchini Cameroon. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo tarehe 6 Novemba 2018, ambapo taarifa za awali zinadai kuwa, wahusika wa utekaji huo ni makundi ya wanamgambo wanaotaka kujitenga na nchi hiyo, hususan kwenye majimbo yanayotumia lugha ya kingereza.
Kwa mujibu wa video inayosambaa katika mitandao ya kijamii, inaonyesha wanafunzi hao wakirundikwa kwenye chumba kimoja bada ya kutekwa nyara, huku waasi wakiwaamuru kutaja majina yao.
Gavana wa jimbo la Kaskazini Magharibi, Adolphe Lele L’Afrique amevishutumu vikundi hivyo vya uasi, wakati serikali ikisema kwamba vyombo vya dola vinaendesha operesheni ya kuwakomboa mateka hao.
Chanzo: BBC Swahili
More Stories
Milioni 91 wapona corona duniani
Papa Francis atembelea Iraq
Kesi mauaji ya Jamal Khashoggi yaanza tena