Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari Mkuu Umoja wa Afrika amwangukia Putin, ‘Afrika ndio wahanga’
HabariKimataifa

Mkuu Umoja wa Afrika amwangukia Putin, ‘Afrika ndio wahanga’

Spread the love

MWENYEKITI wa Umoja wa Afrika (AU), Macky Sall ambaye pia ni Rais wa Senegal amemtaka Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuchukua hatua kutoka na mateso yanayozipata nchi za Afrika kutokana na vita kati ya nchi hiyo na Ukraine.

Amemueleza kuwa Afrika inaathiriwa pakubwa na vita hiyo hususani kutokana na uhaba wa nafaka na mbolea. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Putin jana tarehe 3 Juni, 2022 amekutana na mwenyekiti huyo wa Umoja wa Afrika pamoja na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat katika makazi yake kwenye mji wa pwani wa Sochi.

Rais Sall amesema kuzuiwa kwa bidhaa hizo katika bandari za nchini Ukraine kumeiathiri dunia hasa nchi za Afrika hata kama ziko mbali na kanda vinakofanyika vita lakini nchi hizo ni waathirika katika ngazi ya kiuchumi kutokana na vita hivyo.

Mwenyekiti huyo AU amesema ni muhimu kushirikiana kwa pamoja ili yote yanayohusu chakula, nafaka na mbolea yawe nje ya vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya Urusi baada ya nchi hiyo kuivamia kijeshi Ukraine.

Katika hotuba mbele ya waandishi wa habari, Rais Putin hakutaja moja moja juu ya usafirishaji wa nafaka lakini alisema Urusi siku zote iko upande wa Afrika na sasa ina nia hasa ya kuimarisha ushirikiano wake na bara hilo.

Operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine na msururu wa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Urusi vimetatiza usafirishaji wa mbolea, nafaka ya ngano na bidhaa nyingine kutoka nchi hizo mbili, na hivyo kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula na mafuta, hasa katika mataifa yanayoendelea.

Bei ya nafaka barani Afrika imepanda kwa sababu ya kudorora kwa ununuzi wa nje wa bidhaa kutoka Ukraine na hivyo kuzidisha athari za migogoro na mabadiliko ya hali ya hewa hatua inayozidhisha hofu ya kuongezaka kwa migogoro ya kijamii.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa nchi za Afrika ziliagiza asilimia 44 ya ngano kutoka Urusi na Ukraine kati ya mwaka 2018 na mwaka 2020.

Pia kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika bei ya ngano imepanda kwa karibu asilimia 45 hii ikiwa ni matokeo ya kuzuiwa usafirishaji wa nafaka na bidhaa zingine kutoka Ukraine na Urusi. Nchi hizo ndizo wazalishaji wakuu wa nafaka na mbolea duniani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!