October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkutano wa Trump wadoda Oklahoma

TULSA, OKLAHOMA - JUNE 20: A supporter sits in the upper seats during a campaign rally for U.S. President Donald Trump at the BOK Center, June 20, 2020 in Tulsa, Oklahoma. Trump is holding his first political rally since the start of the coronavirus pandemic at the BOK Center on Saturday while infection rates in the state of Oklahoma continue to rise. (Photo by Win McNamee/Getty Images)

Spread the love

MATARAJIO ya timu ya kampeni ya Donald Trump, Rais wa Marekani katika kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, yanawavunja moyo. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Katika mkutano wake wa kwanza baada ya kumaliza ‘lockdown’ mbele ya watu kiduchu tofauti na matarajio yake, Trump amehutubia katika eneo la Benki ya Tulsa, Oklahoma akisema, kuna kundi la watu wakimfanyia kitu kibaya.

Trump hakufafanua zaidi kundi hilo la watu, wala kitu gani ambacho wamekuwa wakimfanyia.

Awali, Trump alieleza kwamba watu walioomba tiketi za kuhudhuria mkutano huo wa kampeni idadi yao ilikaribia milioni moja, na kuwa ilitarajiwa iweke video mubashara ili watakaozidi, waweze kufuatilia mkutano huo nje ya ukumbi. Hata hivyo, baadhi ya viti vilibaki wazi.

Kwenye hotuba yake iliyodumu kwa takribani saa mbili kwenye eneo hilo kitovu cha Republican, Trump alisema, alisingiziwa kuwa aliagiza kupunguzwa kwa upimaji wa virusi vya corona kwasababu watu wengi walikuwa wakipatikana na virusi hivyo.

Hata hivyo, waliohudhuria mkutano huo wa kampeni, walilazimika kusaini makubaliano ya kuilinda timu ya kampeni ya Trump kwamba, haitawajibika na ugonjwa wowote iwapo watapata maambukizi.

Saa kadhaa kabla ya tukio hilo kuanza, maofisa walisema, wahudumu sita wa kampeni ya Trump walipatikana na maambukizi ya virusi vya corona.

error: Content is protected !!