July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkutano mkuu wa Tamwa kufanyika Jumamosi

Mkurugenzi Mtendaji wa Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA), Valerie Msoka

Spread the love

ZAIDI ya wanachama 100 wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA)- Jumamosi tarehe 28 Machi, 2015, wanafanya mkutano wao mkuu wa mwaka 2014. Anaandika Mwandishi wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka,  pamoja na mambo mengine wanachama watapata fursa ya  kutathmini kazi zilizofanyika mwaka 2014, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2015-2021.

Msoka amesema mkutano huo utaanza saa 2:00 asubuhi katika ofisi za chama zilizoko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo utakaoanza na mafunzo tarehe 27 Machi mwaka huu, utawapa fursa wanachama kujadili mafanikio yaliyopatikana kwenye mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita (2009 -2014).

Pia wanachama watajadili pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji ambapo pia watamchagua Mwenyekiti mpya baada ya aliyekuwepo kumaliza muda wake.

 Taarifa ya Msoka imeongeza kuwa, baada ya mkutano huo, wanachama watajumuika pamoja katika hafla ya kuchangia mfuko wa shughuli za TAMWA (Gala Dinner) ambazo ni pamoja na kupiga vita vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto itakayofanyika jioni katika hoteli ya Serena.

Mkutano mkuu wa TAMWA ndicho chombo cha juu chenye mamlaka ya kurekebisha katiba yake, kuingiza wanachama wapya, kuchagua viongozi, kupitisha ripoti za mwaka na kutoa maamuzi kuhusu mipango na mikakati ya chama kuhusu utetezi.

error: Content is protected !!