May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkutano mkuu CCM Aprili 30, Dk. Samizi …

Spread the love

 

MKUTANO mkuu maalum wa chama tawala nchini Tanzania-Chama Cha Mapinduzi (CCM), utafanyika tarehe 30 Aprili 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lengo la mkutano huo ni kumchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Ni baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake, Dk. John Pombe Magufuli, kufariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.

Mwili wa Dk. Magufuli ambaye pia alikuwa Rais wa Tanzania, ulizikwa nyumbani kwake, Chato mkoani Geita.

Ingawa CCM haijaweka wazi atakayechaguliwa, lakini Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole aliwahi kuwaeleza wanahabari kwamba, atakuwa Rais wa sasa, Samia Suluhu Hassan, ambaye atakwenda kupigiwa kura.

Jana Jumanne, tarehe 30 Machi 2021, kilifanyika kikao cha kamati kuu jijini Dodoma ambacho kiliongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilimpitisha Dk. Florence Samizi kuwa mgombea ubunge wa Muhambwe mkoani Kigoma, katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 2 Mei 2021.

Uchaguzi huo, unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wake, Atashasta Nditiye wa CCM, kufariki dunia kwa ajli ya gari jijini Dodoma tarehe 12 Februari 2021.

Fomu za kuwania jimbo hilo zimekwisha anza kutolewa tangu tarehe 28 Machi hadi 3 Aprili 2021, siku ambayo uteuzi utafanyika na kuanzia kwa kampeni hadi 1 Mei 2021.

error: Content is protected !!