July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkuta: Tufanye siasa za kistaarabu

Spread the love

DANIEL Mtuka, mgombea ubunge katika jimbo la Manyoni Mashariki (CCM), amewataka wagombea uongozi katika uchaguzi mkuu ujao, kufanya siasa za kistaarabu. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Anasema, “…hakuna sababu ya kukashifiana. Ni muhimu tukafanya siasa za kistaarabu; siyo kuhonga wapigakura au kuwanunua. Tukifanya hivyo, tutasababisha kupatikana kwa viongozi wabovu.”

Akizungumza mbele ya msimamizi wa uchaguzi, Mtuka amesema, ni muhimu kufanya siasa zisizogombanisha wananchi.

“Najua kila mtu anatamani kushinda ubunge, lakini jambo la msingi ni kuhakikisha siasa zinazofanyika ni za kistaarabu, kulinda amani, utulivu na mshikamano,” amesisitiza.

Amesema, “Wapo watu ambao wanadhani siasa ni ugomvi, lakini kila mmoja anatakiwa kufanya siasa za kisera na kuwaeleza wananchi atawatumikia vipi wananchi, badala ya kutumia majukwaa kuwatukana wenzake.”

Akizungumzia masuala ya rushwa, Mtuka alisema iwapo wananchi watawachagua viongozi watoa rushwa ni wazi kuwa watashindwa kupata kile walichokusudia kupata kwa maana ya maendeleo.

Kwa upande wake, msimamizi wa uchaguzi huo, Supeet Rone Mseva aliahidi kutenda haki kwa kila mgombea.

Alisema, “Nataka kuwaeleza ndugu zangu wagombea kwamba mimi ni mkurugenzi wa halmashauri ya Manyoni, lakini kwa sasa ni msimamizi wa uchaguzi. Sitampendelea mtu yoyote bali mimi na timu yangu ya uchaguzi tutatenda haki kwa kila mmoja.”

Mtuka amewataka wagombea wote kutumia majukwaa vizuri kwa lengo la kudumisha umoja na mshikamano katika tafa.

error: Content is protected !!