MKURUGENZI wa Taasisi ya Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays anaivuruga taasisi hiyo inayojishughulisha na michezo kwa watu wenye ulemavu wa akili kwa kumuhusisha mtoto wake katika majukumu ya Bodi ya taasisi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Rays anatumia mamlaka yake vibaya kwa kumpeleka mtoto wake huyo katika miradi ya mafunzo yanayotolewa katika mikoa mbalimbali hapa nchini nje ya misingi ya bodi hiyo.
Hivi sasa Rays na mtoto wake wakiwa na watendaji wengine wako katika mikoa ya Tabora na Kigoma wakitoa mafunzo, yakiwemo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu ulipo mkoani Kigoma, uteuzi wa mtoto wake mara zote huufanya bila kuishirikisha bodi.
Mbali ya Mafunzo hayo mikoani, piakatikamichezo ya Taifakwa Walemavu wa akili iliyofanyika jijini Mwanza, miaka miwili iliyopita, alimpa majukumu ya bodi mtoto wake, jambo ambalo lilisababisha malalamiko kwa baadhi ya walimu wa mikoani waliofikisha malalamiko kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Miezi michache iliyopita, BMT iliita bodi na Mkurugenzi wake kwa lengo la kufikisha malalamiko yanayomhusu Rays lakini bado anaendelea na mipango yake ya kutekeleza majukumu bila kushirikisha bodi hasa ya kumteua mtoto wake ambaye ni mmoja wa watangazaji wa televisheni jijini Dar es Salaam.
“Anayoyafanya Rays hayako katika Utawala bora, hivyo tunakerwa na tabia zake hasa kumshirikisha mtoto wake katika majukumu yanayohusu bodi yetu,” alisema mmoja wa watoa taarifa hii na kuongeza
Pia hata baadhi ya Halmashauri zinamlalamikia Rays kwani pamoja na mtoto wake huyo ambaye pia alimpendekeza ahudhurie michezo yaUmoja wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) iliyofanyika mwaka huu mkoani Tabora.
Akijibu tuhuma hizo, Rays alisema hazina ukweli kwani anafanyakazi vizuri na bodi yake nakumtaka mwandishi aendelee kufuatilia zaidi suala hilo kama lina ukweli.
Leave a comment