July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mkurugenzi Rubada aburuzwa kortini

Spread the love

ALOYCE Lukulu, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo Bonde la Mto Rufiji (Rubada), amepandishwa kizimbani leo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za wizi wa Sh. 136 milioni, anaandika Faki Sosi.

Akisomewa shitaka hilo na Denis Lekayokwenye, Wakili wa Serikali mbele ya Warialwande Lema, Hakimu Mkazi Kisutu, la kuiba fedha za mamlaka ya umma, ametuhumiwa kutenda kosa hilo mara tatu.

Mtuhumiwa anadaiwa kuiba Shilingi 50 milioni za Rubada kati ya tarehe 1 hadi tarehe 10 Agosti 2010 kwa kutumia cheo chake.

Lukulu pia anadaiwa kuiba Shilingi 36 milioni kati ya tarehe 1 hadi 30 Novemba mwaka 2010.

Anakabiliwa na kosa lingine la wizi wa fedha za umma Shilingi 50 milioni kwenye mamlaka hiyo.

Mtuhumiwa huyo amerejeshwa rumande kwa kukosa dhamana. Kesi hiyo itaendelea tena 24 Machi mwaka huu.

 

error: Content is protected !!