August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkurugenzi Mkuu UNESCO Duniani atoa ujumbe siku ya Kiswahili duniani

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO duniani, Audrey Azoulay

Spread the love

 

MKURUGENZI Mkuu wa UNESCO duniani, Audrey Azoulay, ameungana na mataifa yote duniani kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani kwa kutuma ujumbe unaosisitiza kutumia maadhimisho hayo kuazimia kujenga na kuimarisha amani pamoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkurugenzi huyo ameeleza kujawa na furaha kuunganika na mataifa mengine duniani katika maadhimisho ya kwanza ya lugha ya Kiswahili duniani “siku ambayo UNESCO inajivunia kuiongoza.”

Azoulay ameyasema hayo katika ujumbe wake, uliosomwa leo tarehe 7 Julai, 2022, katika maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani ambayo kitaifa hapa Tanzania yamefanyika jijini Dar es Salaam mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais Dk Philp Mpango.

Amesema Mkutano Mkuu wa 41 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliidhinisha siku ya tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa ni siku ya kiswahili duniani.

“Kwa kufanya hivyo lugha hii tunaiheshimisha pamoja na kuthamini matumizi ya lugha mbalimbali kwani hicho ni kipaumbele kwa UNESCO,” amesema.

Ameongeza Kiswahili ni lugha inayotumika kuibua fursa mbadala inayolenga kukidhi mtazamo wa dunia kwa ujumla.

“Kukua kwa lugha hii kunatupa historia ya karne ya mabadiliko katika dunia,” amesema Azoulay katika ujumbe wake.

Amesema Kiswahili ni miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa zaidi duniani na kujenga utengamano miongoni mwa jamii na mataifa mbalimbali, lugha ya kurusha habari na lugha ya elimu.

AmesemakKama lugha ya kidiplomasia na kama lugha rasmi ya Umoja wa Afrika, Kiswahili kinachangia kusukuma ajenda ya Afika 2063 ambayo pia ni kipaumbele kwa UNESCO.

“Kwa urithi wa kitamaduni inayowakilisha, ujumbe inaoeneza, mianya ya mawasilinao inayoziba, elimu inayotoa na kuimarisha umoja, lugha ya Kiswahili huchangia kuleta utengamano na amani na UNESCO ina jukumu la kuimarisha na kuleta amani duniani kwahiyo leo kupitia maadhimisho ya siku ya Kiswahili tuazimie kujenga na kuimarisha amani pamoja,” amesema Azoulay.

error: Content is protected !!